
Gundua Kusudi la Maisha yako
UTANGULIZI.
Maisha yasiyo na kusudi ni maisha yanayochosha sana. Ni maisha yasiyokuwa na dira na ni Maisha ya kubahatisha. Mtu asiye na kusudi katika maisha yake hawezi kupima kama amefanikiwa au amefeli katika maisha yake. Mtu wa namna hii anaishi alimradi ameishi. Lengo la kuishi linakuwa ni kuimaliza siku iliyopo na kuianza kesho tena.
Kama alivyo mtengenezaji wa kitu kingine chochote, wakati Mungu anamuumba mwanadamu alikuwa na kusudi la huyo mwanadamu kufanya jambo fulani katika maisha yake. Hakuna manufacturer yeyote anayetengeneza kitu pasipo kwanza kuwa na picha ya kazi/kusudi ya hicho kitu.
Na kama ilivyo kwa vifaa vyovyote vilivyotengenezwa mfano wa simu au gari huwa vinakuwa na makusudi ya jumla na makusudi maalum, vivyo hivyo kwa wanadamu na sisi pia tuna makusudi ya jumla na makusudi mahususi katika maisha yetu. Kusudi la jumla na kuu la simu ni kuwasiliana lakini pia kila aina ya simu na toleo katika aina ya simu huwa lnakusudi maalumu.simu ya button(kitochi) na simu janja (smartphone) zote ni simu na zote kusudi lao kuu ni kuwasiliana lakini ni ukweli usiopingika kuwa simu janja inakusudi mahususi zaidi hata katika huko kuwasiliana kwake.
Kama wewe ni mtumiaji wa simu tayari umeshaanza kuona tofauti ya simu janja na simu ya button, tayari kwa haraka sana umeshaona ni kwa kiasi gani aliye na simu janja ana-enjoy programu kama whatsapp, facebook,instagram n.k wakati yule mwenye simu ndogo ya button kwake mawailiano ni kupiga na sms.
Lakini ni ukweli mwingine kuwa hata hizo simu janja zinatofautiana kwa viwango vya juu sana.kuna mambo mengi sana katika simu yanayotofautisha simu moja na simu nyingine, kuanzia ubora wa mawasiliano, ubora wa picha, ukubwa wa kuhifadhi data n.k.
Na ukweli ni kwamba kila aina na kila toleo la simu lina kusudi tofauti la kutimiza katika kuishi kwake na mara nyingi tunamiliki hizi simu pasipo kujua kusudi mahsusi la simu husika na hivyo kufanya tutumie simu zote kwa kusudi lile la jumla na sio kusudi mahususi.
Kwa upande mwingine wewe mwenyewe ni shahidi kuwa baadhi ya simu matumizi yanayotumiwa kwayo sio matumizi ya msingi wala matumizi Mahususi. Mfano mtoto anapoiona simu, kwake hiyo ni game au tv. Kwa mtoto, simu sio kifaa cha mawasiliano bali ni kifaaa cha kuchezea game na kuangalia picha au video.
Hali hii tunayoiona kwenye kifaa simu inashabihiana sana na kwa wanadamu. Mwanadamu alipoumbwa alikuwa na kusudi la jumla(msingi) na pia kila mwanadamu anakusudi mahususi katika maisha yake.
Lengo la kozi hii ni kuangazia kusudi mahususi ambalo Mungu amekuumba kwalo, je wewe ni toleo lipi la mwanadamu, je Mungu amewekeza nini kwako na anataka uishi maisha gani na kutimiza kusudi gani maishani?
Je wewe mi mfano wa simu ya button au smart phone?, kama ni smart phone, ni ya aiana gani na toleo lipi, nini ubora uliowekwa ndani yako na Mtengenezaji wako anatarajia nini kutoka kwako?
Haya ni kati ya maswali ambayo mtu lazima ajiulize awapo duniani, na ukiondoka pasipo kujiuliza na kupata majibu basi utakuwa ni kati ya watu ambao hawajatendea haki kabisa maisha uliyopewa na Mungu.
Kwa hiyo mpaka hapa tayari tumeshafahamu kuwa kuna kusudi la jumla la kila mwanadamu na kuna kusudi mahususi la kila mwanadamu.
Nitakuwa nimefanikiwa sana kama nitaweza kukusaidia kujua kusudi la maisha yako, lile la jumla na lile mahususi ambalo Mungu anatazamia uliishi uwapo hapa duniani na ni imani yangu kwamba utakapomaliza kozi hii utafanikiwa kufahamu kusudi la jumla na mahususi la maisha yako.
Si hivyo tu, bali utakuwa pia umefahamu kwa hakika nini cha kufanya kila siku ili kulitimiza hilo kusudi lako.
Mungu akubariki sana tunapoendelea kujifunza.
Curriculum
- 7 Sections
- 16 Lessons
- 5 Quizzes
- 0m Duration
UTANGULIZI
- Kusudi la Jumla la Mwanadamu.
- Kusudi Mahususi la Mwanadamu.
- Assignment 1: Kusudi la Mwanadamu
JE MIMI NI NANI?
- Je mimi ni nani?
- Maswali ya kujitathmini na kujitafuta
- Matokeo ya Tathmini
NDOTO ZANGU NA UWEZO WANGU WA KIPEKEE
- Fahamu uwezo wako wa Kipekee
- Maswali ya Kutathmini Uwezo wa Kipekee.
- Matokeo ya Tathmini.
- Zoezi la Vitendo No 1_Ndoto Zangu
KUWEKA MAONO YA MAISHA YANGU.
- Mambo ya kuzingatia wakati wa kuandika Maono ya Maisha yako.
- Assignment 2_ Maono ya Maisha Yangu.
- Zoezi la Vitendo No 2_Maono Yangu
DHIMA (MISSION) YA MAISHA YANGU.
- Hatua za Kuandika Dhima ya Maisha Yako:
- Dhima (Mission) ya Maisha yako ni nini?
- Assignment 3_Dhima ya Maisha Yangu
- Zoezi la Vitendo No 3_Dhima Yangu
NAMNA YA KUWEKA MALENGO YA MAISHA YANGU
- Zoezi la vitendo Na 4_Malengo Yangu.
MWONGOZO WA KUANDIKA MPANGO KAZI:
- Umuhimu wa Kupanga
- Jinsi ya Kuandika Mpango kazi
- Zoezi la vitendo Na 5_Mpango Kazi Wangu